Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 26 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 345 2024-05-15

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:-

Je, upi mpango wa kuwasaidia wakulima wa tumbaku kupata vitendea kazi mapema na kupunguza bei vikiwemo Jute Twine na Cotton Twine?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta, Mbunge wa Urambo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kuanzia 2020/2021 hadi 2023/2024 upatikanaji wa pembejeo za tumbaku umekua kwa kiwango kinachoridhisha. Aidha, changamoto ya upatikanaji wa Jute twine na Cotton Twine umejitokeza katika msimu wa 2023/2024 ambapo pembejeo hizo zilichelewa na msingi wa ucheleweshwaji huo ni benki kuchelewa kutoa letter of credit.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutatua changamoto hii, Serikali inaendelea kuhamasisha makampuni ya ndani yawekeze kwenye uzalishaji wa ndani wa kamba na magunia. Aidha, Serikali imeandaa utaratibu wa kutumia Bodi ya Tumbaku, Kampuni yetu ya Serikali ya TFC na Muungano wa Vyama Vikuu vya Ushirika – TCJE kuagiza pembejeo za misimu miwili miwili. Lengo ni kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo za zao kwa wakati.