Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 30 Policy, Coordination and Parliamentary Affairs Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu 390 2024-05-21

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: -

Je, lini zoezi la kuhamia Dodoma litakamilika na Taasisi ngapi zimeshahamia Dodoma?

Name

Ummy Hamisi Nderiananga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, zoezi la kuhamisha Makao Makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma lilianza rasmi mnamo mwaka 2016. Hadi sasa jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali Kuu, Bunge, Mahakama, vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na taasisi 65 wameshahamia Dodoma na wanaendelea kutekeleza majukumu yao wakiwa Makao Makuu ya Nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatarajia kukamilisha mpango wake wa kuhamia Makao Makuu ya Nchi, Dodoma kwa kuzingatia mpango kazi maalum na ujenzi wa awamu ya pili wa majengo ya Ofisi za Wizara na Taasisi utakaohitimishwa ifikapo mwaka 2025.