Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 9 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 137 | 2024-09-06 |
Name
Dr. Josephat Mathias Gwajima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kawe
Primary Question
MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha barabara za vumbi za Jimbo la Kawe zilizoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha zinachongwa?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imechukua hatua za haraka kukabiliana na uharibifu mkubwa uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni katika barabara za udongo za Jimbo la Kawe.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuhakikisha usalama na ufikikaji wa barabara hizi muhimu za usafiri, Serikali imefanya matengenezo ya barabara za Jimbo la Kawe kwa kuchonga baadhi ya barabara hizo ambazo zimeathiriwa na mvua. Jumla ya kilometa 66.32 za barabara tayari zimechongwa ambapo gharama zilizotumika mpaka sasa ni shilingi milioni 136.68.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na kazi za ukarabati wa barabara zote zilizoathirika na mvua ili kuzirejesha katika hali yake ya awali kulingana na upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved