Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 9 | Information, Culture, Arts and Sports | Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo | 147 | 2024-09-06 |
Name
Stella Simon Fiyao
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga Uwanja wa Michezo Wilayani Ileje?
Name
Dr. Advocate Damas Daniel Ndumbaro
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Songea Mjini
Answer
WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, jukumu la ujenzi wa miundombinu ya michezo ni la Serikali ikiwemo Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya michezo, taasisi, mashirika na watu binafsi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Serikali ipo katika ukarabati wa viwanja vya Benjamin Mkapa pamoja na Uhuru Jijini Dar es Salaam, ujenzi wa uwanja wa Arusha na ukarabati viwanja vingine vitano vya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya CHAN 2025 na AFCON 2027.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo basi, Serikali inaishauri Halmashauri na Wilaya ya Ileje kutenga fungu katika bajeti yake ili kutekeleza mradi ya ujenzi wa kiwanja cha michezo wakishirikiana na wadau wa maendeleo. Wizara ipo tayari kuwapatia wataalamu wa miundombinu ya michezo kuwashauri ipasavyo na itakapofika hatua ya utekelezaji mradi wa ujenzi wa uwanja huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia Bunge lako Tukufu nazipongeza Halmashauri za Wilaya za Kinondoni kwa kujenga Uwanja wa KMC, Bukoba Mjini kwa kujenga Uwanja wa Kaitaba, Nyamagana kwa kujenga Uwanja wa Nyamagana, Halmashauri ya Mji-Babati kwa kuwanja Uwanja wa Tanzanite na Halmashauri ya Namungo kujenga Uwanja wa Majaliwa Stadium) kwa kuonyesha mfano bora na sasa wanamiliki na kuendesha viwanja vya michezo vya kisasa. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved