Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 9 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 73 | 2024-09-02 |
Name
Mwanakhamis Kassim Said
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Magomeni
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO K.n.y. MHE. MWANAKHAMIS KASSIM SAID aliuliza:-
Je, Serikali haioni haja ya kuweka usiri katika ugawaji wa taulo za kike shuleni na vyuoni ili kudumisha silka na utamaduni wa Mtanzania? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, inatambua vyema mila, desturi na utamaduni wa nchi yetu kuhusu suala la hedhi salama. Utafiti uliofanywa na NIMR Mwaka 2021 ulibaini kwa kiasi kikubwa wanafunzi wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo kutokana na ukosefu wa bidhaa za hedhi kwa siku tano hadi siku saba kwa mwezi, sawa na siku 50 au 70 kwa muda wa masomo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaweka jitihada kuhakikisha jamii inatambua umuhimu wa hedhi salama na kusaidia upatikanaji wa vifaa vya hedhi kwa wasichana. Lengo ni kuwezesha uwepo wa vifaa sahihi vya kujisitiri, upatikanaji wa maji safi, sabuni pamoja na sehemu sahihi ya kuhifadhia au kutupa vifaa ambavyo tayari vimetumika. Serikali itaendelea kuzingatia suala la usiri kwa kuhakikisha kuwa, kunakuwa na chumba maalum shuleni kwa wanafunzi wa kike kujisitiri wakati wa hedhi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved