Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 5 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 76 | 2024-09-02 |
Name
Neema Gerald Mwandabila
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza:-
Je, nini mkakati wa Serikali kufanya utafiti kwa mazao ya kilimo na biashara ili kubaini uwepo wa changamoto katika msimu husika? (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Neema Gerald Mwandabila, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Kilimo kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inaendelea kufanya survey za changamoto zinazokabili uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, hasa afya ya udongo, magonjwa na wadudu ili kubaini viashiria vya hatari kwa msimu husika na kutoa ushauri kwa wadau wa kilimo.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imeendelea kuitengea TARI bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 31, kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu mbalimbali, ununuzi wa vifaa vya kisasa na mafunzo kwa wataalam wa maabara na watafiti ili kuendelea kugundua teknolojia mbalimbali zinazokabiliana na mabadiliko ya tabia-nchi, hususan afya ya udongo, mbegu zinazohimili ukame, wadudu na magonjwa. Aidha, Serikali itaendelea kusambaza kwa wakulima teknolojia zinazogunduliwa na watafiti ili waweze kutambua zinazofaa katika msimu husika. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved