Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 38 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 494 | 2024-05-31 |
Name
Rose Cyprian Tweve
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza: -
Je, kigezo cha mtihani wa kuandika kabla ya kujiunga na Vyuo vya Ufundi (VETA) ni cha lazima kwa wanafunzi wa mafunzo kwa vitendo?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) inatoa mafunzo ya ufundi stadi kwa nadharia kwa 30% na vitendo kwa 70%.
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa stadi za kuandika, kusoma na kuhesabu katika utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) hutoa mitihani ya majaribio (aptitude test) wa kujiunga kwenye vyuo vyake. Hii ni kwa sababu kuna umuhimu wa kubaini endapo wanaotaka kujiunga na vyuo vya VETA wanamudu stadi za KKK ikiwa ni kigezo cha kujiunga na vyuo vya ufundi stadi na pia kwa ajili ya muendelezo wa kielimu kwa hapo baadae pindi mwanafunzi akihitaji kujiendeleza zaidi. Ninakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved