Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 38 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 495 2024-05-31

Name

Emmanuel Adamson Mwakasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kuimarisha upatikanaji wa mtandao wa simu katika kata 29 za Tabora Mjini?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imejenga minara ya mawasiliano ya simu saba katika Jimbo la Tabora Mjini. Minara hiyo ilijengwa na Vodacom na Halotel katika Kata za Itetemia, Kabila, Kalunde, Ndevelwa, Tumbi na Uyui kupitia awamu mbalimbali za miradi iliyotekelezwa kati ya Agosti, 2017 na Januari, 2020.

Mheshimiwa Spika, kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidigitali Kata za Ifucha na Kiloleni zitajengewa minara na kampuni ya Honora (Tigo). Kwa upande wa Kata ya Kakola UCSAF imeingia mkataba na TTCL kwa ajili ya kujenga mnara katika kata hiyo. Utekelezaji wa mradi huu ni miezi 24 kuanzia tarehe 13 Mei, 2023.

Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa miradi inayoendelea, Serikali kupitia UCSAF itafanya tathmini ya hali ya mawasiliano katika Jimbo la Tabora Mjini ili kubaini maeneo yenye uhitaji wa kufikishiwa mawasiliano.