Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 38 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 496 | 2024-05-31 |
Name
Zuena Athumani Bushiri
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga majosho na malambo katika Kata za Bendera, Kalemawe na Maore katika Jimbo la Same Mashariki?
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa majosho na malambo nchini ili kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na wadudu na kuongeza upatakanaji wa maji kwa ajili ya mifugo. Katika mwaka wa fedha 2023/2024 Wizara inaendelea na ujenzi wa majosho 246 kwa gharama ya shilingi bilioni 5.6 na kusambaza dawa za ruzuku za kuogesha mifugo lita 56,000 nchi nzima. Pia ujenzi wa malambo na visima virefu kwa ajili ya maji ya mifugo unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea na ujenzi wa majosho na malambo yakiwemo ya Jimbo la Same Mashariki kwa kadiri ya upatikanaji wa fedha. Hivyo natoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Same kuainisha maeneo yanayofaa kwa ujenzi wa malambo katika kata hizo, kufanya usanifu na kuwasilisha gharama zake Wizarani ili yaweze kujumuishwa katika mpango wa bajeti ya Wizara wa mwaka 2025/2026 kadiri ya upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Spika, pia naomba kutoa wito kwa wafugaji na wadau wengine hapa nchini kuungana na Serikali kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu ya maji ili kusaidia kupunguza changamoto ya maji kwa mifugo hapa nchini, ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved