Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 50 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu | 642 | 2024-06-20 |
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza:-
Je, ni lini wazee wanaostaafu watapata mafao yao kwa wakati?
Name
Deogratius John Ndejembi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chamwino
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Shabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Lushoto, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, mafao ya pensheni kwa wastaafu yanalipwa kwa mujibu wa Sheria zinazosimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambapo zinaelekeza mifuko kulipa mafao ndani ya siku 60 tangu mwanachama anapostaafu. Kwa sasa, mifuko imeboresha mifumo yao na wastaafu wote wanalipwa mafao yao kwa wakati ndani ya siku 60.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved