Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 50 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 644 | 2024-06-20 |
Name
Yahya Ally Mhata
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itanunua Magari ya Wagonjwa, kwa ajili ya Vituo vya Afya vya Nanyumbu, Michiga na Mtambaswala?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu imepelekewa magari mawili Novemba 2023, moja la kubeba wagonjwa na jingine la usimamizi shirikishi. Aidha, gari la kubeba wagonjwa lipo Hospitali ya Wilaya na linatumika kufuata wagonjwa wa dharura kwenye Vituo vya afya vya Nanyumbu, Michiga na Mtambaswala.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inakusudia kuongeza gari jingine la kubebea wagonjwa, ili kuwezesha huduma za rufaa za ndani na nje ya Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu. Aidha, Serikali itaendelea kutafuta fedha, kwa ajili ya kununua magari ya kubebea wagonjwa katika Halmashauri zenye upungufu, ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved