Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 50 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 650 | 2024-06-20 |
Name
Ameir Abdalla Ameir
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. ABDUL YUSUF MAALIM K.n.y. MHE. AMEIR ABDALLAH AMEIR aliuliza:-
Je, ni kwa kiwango gani TEHAMA inatumika kuboresha sekta ya kilimo nchini?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, matumizi ya TEHAMA katika sekta ya kilimo ni mojawapo ya njia muhimu za kuboresha uzalishaji, ufanisi na tija kwa wakulima. Matumizi ya mifumo hiyo yamesaidia kufanya usajili wa taarifa za wakulima na kutumia taarifa na takwimu hizo kutoa huduma nyingine, mathalan utoaji wa mbolea kwa mpango wa ruzuku, kutoa huduma za ugani kupitia Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Wizara (Kilimo Call Centre) na Mobile Kilimo, ambapo wakulima wanapata ushauri wa kitaalamu kwa kujibiwa maswali yao na hivyo kutatua changamoto zinazowakabili na kuboresha uzalishaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile TEHAMA imesaidia katika utoaji wa vibali mbalimbali vikiwemo vibali vya kuingiza na kusafirisha mazao na bidhaa za kilimo ndani na nje ya nchi na kufanya malipo kwa wakati lakini imewezesha wakulima kupata taarifa za masoko kwa urahisi na hivyo kuwawezesha kuuza mazao yao kulingana na bei ya soko. Pia, kuwawezesha wakulima kupata taarifa za hali ya hewa kwa wakati, ambazo ni muhimu sana katika kupanga shughuli za kilimo kama vile upandaji na uvunaji, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved