Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 22 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 288 | 2024-05-09 |
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Primary Question
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga miundombinu ya Shule ya Sekondari Mkugwa ikiwemo Mabweni, Bwalo na Madarasa, Muhambwe?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Shule ya Sekondari Mkugwa ina jumla ya wanafunzi 546, kidato cha tano wapo 377 na kidato cha sita 169. Vyumba vya madarasa vinavyohitajika ni 14 na vyumba vilivyopo ni 14 hivyo, hakuna upungufu. Mabweni yanayohitajika ni nane, yaliyopo ni saba na upungufu ni bweni moja. Juhudi zinafanywa na Halmashauri ya Kibondo kutafuta fedha za kuongeza bweni moja, ili kuondokana na upungufu uliopo.
Mheshimiwa Spika, shule haina bwalo wanafunzi wanatumia jengo lililokuwa la sanaa na maonyesho katika eneo ilipokuwa kambi ya wakimbizi. Jengo hili ni dogo likilinganishwa na wanafunzi 546 waliopo shuleni kwa sasa.
Mheshimiwa Spika, kuanzia Mwaka 2025/2026 Serikali itaendelea kutenga fedha za kujenga bwalo na miundombinu mingine kila mwaka wa fedha katika shule zisizokuwa na bwalo kwa kuanzia na Shule ya Sekondari ya Mkugwa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved