Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 22 | Union Affairs | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 290 | 2024-05-09 |
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa Kingo za Mto Msuka Ilemela utakamilika ili kuepusha vifo vya mara kwa mara pindi mvua zinaponyesha?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa Kingo za Mto Msuka unaendelea ambapo hadi sasa ujenzi wa daraja na kingo zake zenye urefu wa takribani meta 500 umekamilika. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Manispaa ya Ilemela kupitia Mradi wa Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia imeomba kiasi cha shilingi bilioni 6.7 kwa ajili ya ujenzi wa barabara na kukamilisha ujenzi wa Kingo za Mto Msuka ambapo ujenzi wake utaendelea baada ya fedha hizo zilizoombwa kupatikana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved