Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 1 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu | 1 | 2024-08-27 |
Name
Dr. Faustine Engelbert Ndugulile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kigamboni
Primary Question
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO K.n.y. MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: -
Je, lini NSSF itakamilisha makusanyo ya deni la ujenzi wa Daraja la Nyerere - Kigamboni na kulikabidhi Serikalini?
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Faustine Engelbert Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni, ambaye sisi Watanzania wote tunaungana kumtakia kila la heri katika uchaguzi unaoendelea na tuna imani Mwenyezi Mungu ataweka mkono wake wa heri na tutashinda.
Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulianza rasmi uendeshaji wa Daraja la Nyerere Kigamboni mwezi Mei 2016 ambapo hadi kufikia mwezi Julai 2024 sawa na miaka tisa ya uendeshaji, jumla ya shilingi 102,018,000,000 zimekusanywa kutokana na tozo mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taarifa ya upembuzi yakinifu wa mradi wakati wa kuanzishwa kwake, mradi utarejesha fedha za mfuko kiasi cha shilingi bilioni 344 hadi kukamilika kwake kwa kipindi cha miaka 30. Fedha hizi ni gharama za uendeshaji pamoja na ulinzi na thamani ya fedha iliyowekezwa. Hivyo, baada ya fedha hizo kurejeshwa, mradi utakabidhiwa Serikalini.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved