Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 2 2024-08-27

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga uzio katika Kituo cha Afya Pasua Manispaa ya Moshi?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Mfuko wa Jimbo imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa Kituo cha Afya cha Pasua. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 hadi 2023/2024, jumla ya shilingi milioni 16 zilitolewa na kujenga kipande cha urefu wa mita 65 kati ya urefu wa mita 242 wa uzio huo.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Manispaa ya Moshi imetenga shilingi milioni 25 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa uzio huo. Aidha, Serikali kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Moshi itaendelea kutenga bajeti ya ujenzi wa uzio huo hadi utakapokamilika, ahsante. (Makofi)