Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 1 Planning and Investment Ofisi ya Rais: Mipango na Uwekezaji 5 2024-08-27

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza:-
Je, faida gani Serikali imepata kwa kuanzisha miradi mingi kwa wakati mmoja bila kusubiri mingine ikamilike ili kuanza mipya?

Name

Stanslaus Haroon Nyongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Maswa Mashariki

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Anatropia Lwehikila Theonest, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikiibua na kutekeleza miradi/programu mbalimbali za maendeleo kwa kuzingatia malengo na shabaha za Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano. Ili kuhakikisha kasi ya utekelezaji wa programu na miradi inafikia malengo na shabaha ya Mpango, katika mwaka 2024/2025 msukumo mkubwa umewekwa kwenye kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kielelezo pamoja na kukamilisha utekelezaji wa programu na miradi ya maendeleo hususan katika sekta wezeshi ambayo ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji.

Mheshimiwa Spika, aidha, miradi mipya itakayojumuishwa kwenye Mpango ni ile inayolenga kuleta matokeo ya haraka ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, kuongeza wigo wa ujumuishi wa Watanzania, kuongeza uwiano wa mapato ya ndani na pato la Taifa, kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma za nje ili kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni na kuongeza ajira hapa nchini.