Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 1 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 12 2024-08-27

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha uzalishaji wa zao la korosho katika Wilaya ya Nanyumbu?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wa zao la korosho kwa uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla, Serikali imeendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuboresha uzalishaji wa zao la korosho nchini ikiwemo Wilaya ya Nanyumbu kwa kusimamia huduma za ugani ambapo Maafisa Ugani wote 16 wamepatiwa pikipiki ili kuhakikisha wakulima wanafikiwa kwa wakati na kupatiwa elimu stahiki, ikiwemo kanuni bora za kilimo cha korosho ikijumuisha matumizi sahihi na salama ya viuatililifu.

Mheshimiwa Spika, vile vile, kuendelea kuboresha kanzidata ya wakulima wa korosho na kutoa ruzuku ya pembejeo kwa lengo la kuhakikisha kipato cha wakulima kinaongezeka kwa kupunguza gharama za uzalishaji.

Mheshimiwa Spika, kutokana na utekelezaji wa mipango hiyo, uzalishaji wa korosho katika Wilaya ya Nanyumbu unaendelea kuongezeka kutoka tani 15,735 mwaka 2021/2022 na kufikia tani 16,735.027 mwaka 2023/2024 na korosho zote ziliuzwa kwa daraja la kwanza.

Mheshimiwa Spika, malengo yaliyopo ni kuhakikisha uzalishaji katika Wilaya ya Nanyumbu unafikia tani 71,600 ifikapo mwaka 2030 na kuendelea kulinda ubora wa korosho hizo kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi. (Makofi)