Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 9 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 109 | 2024-04-18 |
Name
Martha Festo Mariki
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza:-
Je, kuna mpango gani wa kujenga hosteli za wanafunzi katika shule zilizopo pembezoni mwa Mkoa wa Katavi?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa uwepo wa hosteli katika shule za sekondari za pembezoni mwa Mkoa wa Katavi katika kuwawezesha wanafunzi kuhudhuria masomo kwa muda wote bila vikwazo. Serikali itaendelea na mpango wake wa sasa wa kuhamasisha wananchi kushirikiana na halmashauri kujenga hosteli katika shule za sekondari zenye uhitaji huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutumia fursa hii kumpongeza Mbunge, Mheshimiwa Martha Festo Mariki na wananchi wa Katavi, kwa jitihada wanazoendelea kuzifanya za kujenga hosteli ambapo kwa sasa kati ya shule za sekondari za kutwa 64 zilizopo Mkoani Katavi, wananchi wameweza kujenga hosteli kwenye shule za sekondari 17.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa, kipaumbele cha Serikali ni kujenga mabweni kwenye shule za kidato cha tano ili wanafunzi wote waliofaulu mtihani wa kidato cha nne waweze kupata fursa ya kujiunga na kidato cha tano Julai, 2024.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved