Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 9 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 117 2024-04-18

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kufanya maboresho ya minara iliyojengwa na Halotel Liwale ili iweze kufanya kazi kama ilivyokusudiwa?

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Answer

WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zuberi Mohamedi Kuchauka, Mbunge wa Liwale, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, ilifanya tathmini katika Jimbo la Liwale na kubaini uwepo wa changamoto za mawasiliano katika Minara ya Halotel. Minara hiyo inatakiwa kuongezewa teknolojia 3G na 4G ambapo utekelezaji wake utafanyika kwa kadiri ya upatikanaji wa fedha. Kampuni ya Halotel ina jumla ya minara nane katika Wilaya ya Liwale, ambayo ina uhitaji wa kuiongezea nguvu kutoka 2G kwenda teknolojia ya 3G na 4G. Kiasi cha ruzuku inayohitajika kuiongezea nguvu minara hiyo, ni takribani shilingi 320,000,000 za Kitanzania. (Makofi)