Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 2 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 33 2024-08-28

Name

Mwantumu Mzamili Zodo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MWANTUMU M. ZODO aliuliza:-
Je, upi mkakati wa Serikali kukabiliana na vitendo vya ukatili vinavyoendelea nchini hasa kwa wanawake na watoto?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Baadhi ya mikakati inayotekelezwa ni pamoja na:-

(i) Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Ulinzi na Usalama wa Mtoto umewasilishwa Bungeni na Kusomwa kwa Mara ya Kwanza;

(ii) Mpango kazi wa Taifa wa Awamu ya Pili wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA II) umezinduliwa Mei, 2024;

(iii) Elimu kwa umma imeimarishwa kwa ushirikiano na Maafisa Polisi ngazi ya Kata. Pia, kimeanzishwa Kituo cha Huduma kwa Wateja Wizarani (Call Centre) ili kuongeza nguvu ya elimu kwa umma na kupokea taarifa za vitendo vya ukatili;

(iv) Huduma za madawati ya Jinsia na Watoto zinapatikana katika vituo vyote vya Jeshi la Polisi. Pia, idadi ya Vituo vya huduma ya dharura na jumuishi kwa manusura wa ukatili imeongezeka na kufikia vituo 26 nchini;

(v) Aidha, programu ya elimu ya malezi na makuzi chanya ya maendeleo ya awali ya mtoto inatekelezwa kwenye mikoa na halmashauri zote nchini na pia; na

(vi) Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Wizara ilipata kibali cha ajira kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii 800 na Maafisa Ustawi wa Jamii 350.

Mheshimiwa Spika, ahsante.