Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 2 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 36 2024-08-28

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:-

Je, lini zabuni ya ujenzi wa Barabara ya Mbambo – Ntaba hadi Ipinda kwa kiwango cha lami itatangazwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Mbambo – Ntaba hadi Ipinda yenye urefu wa kilometa 18.13. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.