Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 53 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 677 2024-06-25

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza:-

Je, Serikali haioni haja ya kuongeza umri wa Vijana kufikia miaka 40 kutokana na changamoto wanazopitia?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, AJIRA, KAZI NA WATU WENYE ULEMAVU alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2007 na Mikataba Mbalimbali ya Kimataifa ambayo Tanzania imeridhia kama vile Mkataba wa Vijana wa Afrika wa Mwaka 2006 (African Youth Chater 2006), Sera ya Vijana ya Afrika Mashariki na Azimio la SADC kuhusu Maendeleo na Uwezeshwaji wa Vijana la Mwaka 2015 (SADC Declaration on Youth Development and Empowerment) inatambua kuwa umri wa kijana kwa Tanzania ni kati ya miaka 15 hadi 35.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na sababu hizo, Serikali kwa sasa inaona ni muhimu kuendelea na tafsiri hii ya umri kwa vijana kama inavyotambuliwa na Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana.