Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 53 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 680 2024-06-25

Name

Shamsia Aziz Mtamba

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO K.n.y. MHE. SHAMSIA A. MTAMBA aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha Ujenzi wa Kituo cha Afya Mkunwa - Mtwara Vijijini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Mkunwa kilianza ujenzi mwaka 2019/2020 ambapo ujenzi wake ulianza kwa ramani ya majengo ya hospitali. Aidha, jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimeishatolewa kwa ajili ya ujenzi wa majengo saba (7); jengo la OPD, jengo la wazazi, jengo la dawa, jengo la maabara, jengo la mionzi, nyumba ya mtumishi na kichomea taka. Majengo haya yapo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi na ili kukamilika, kiasi cha shilingi milioni 900 kinahitajika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ukamilishaji wa majengo hayo. Ahsante. (Makofi)