Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 53 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 690 2024-06-25

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza Mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji Kata ya Kitulo kwa wakulima wa viazi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanzisha mkakati wa muda mrefu wa kuwawezesha wakulima wadogo wa viazi Mkoa wa Njombe kwa kuwawekea miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba yao. Kabla ya kujenga miundombinu hii, taratibu za kawaida za kujenga mradi huwa zinafuatwa, ikiwemo kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa maeneo husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea kutambua maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji nchini, ikiwemo yale yanayolimwa zao la viazi. Katika mwaka wa fedha 2024/2025, wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji watatembelea Kata ya Kitulo ili kubaini maeneo yanayofaa kwa shughuli za umwagiliaji na kuyaingiza kwenye mpango wa ujenzi.