Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 53 | Industries and Trade | Wizara ya Viwanda na Biashara | 691 | 2024-06-25 |
Name
Esther Edwin Maleko
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y. MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: -
Je, upi mkakati wa Serikali kuongeza mauzo ya nyama nje ya nchi?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ili kuhakikisha mauzo ya nyama nje ya nchi yanaongezeka. Mikakati hiyo ni pamoja na ukamilishaji wa mkakati wa mauzo nje ya nchi. Serikali kuendelea kuongeza bajeti ya kuboresha sekta ya mifugo, kuvutia uwekezaji wa uongezaji thamani katika sekta ya mifugo, kutumia Balozi zetu kutafuta masoko kwa kufanya majadiliano na nchi zenye uhitaji wa nyama na upatikanaji na ukamilishaji wa michakato ya kupata ithibati mbalimbali zinazokubalika Kimataifa, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved