Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 1 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 11 | 2024-10-29 |
Name
Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba kusini
Primary Question
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga jengo la Kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Muleba?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuimarisha majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kujenga majengo mapya na kukarabati yaliyochakaa. Kutokana na uhaba uliopo wa majengo ya Mahakama, majengo hayo yanajengwa na kukarabatiwa kwa awamu kwa kuzingatia mpango wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya Mahakama kadri fedha zinavyopatikana.
Mheshimiwa Spika, jengo la kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Muleba limepangwa kujengwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved