Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 1 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 18 | 2024-10-29 |
Name
Eric James Shigongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buchosa
Primary Question
MHE. ERICK J. SHIGONGO aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Soko la Samaki la Nyakarilo – Buchosa?
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa soko hilo la samaki, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa Wizara inaendelea na jitihada za kujenga, kuboresha na kukamilisha masoko mbalimbali ya samaki hapa nchini likiwemo soko la Samaki la Nyakarilo kulingana na upatikanaji wa fedha. Aidha, ninaielekeza Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa kuweka ujenzi wa masoko ya samaki kwenye miradi yake ya kimkakati kwa kutenga fedha kupitia mapato yake ya ndani.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved