Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 7 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 107 | 2024-09-04 |
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:-
Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kujenga Barabara ya Sadala - Uswaa kwa kiwango cha lami?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2023/2024, barabara hiyo ilifanyiwa matengenezo ya sehemu korofi kwa gharama ya shilingi milioni 26.8 na mwaka 2024/2025, Shilingi milioni 35 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya maeneo korofi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini katika mwaka 2024/2025 imepanga kufanya usanifu wa kina kwa kilomita zote 9.87 za Barabara hii ya Sadala - Uswaa kwa lengo la kutambua gharama halisi zitakazotumika katika kuijenga. Hata hivyo, mara baada ya usanifu kukamilika na gharama halisi za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved