Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 7 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 108 2024-09-04

Name

Michael Constantino Mwakamo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Vijijini

Primary Question

MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara ya kuunganisha Kongani ya Viwanda ya Kwala na Stesheni ya SGR ya Ruvu?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini imepanga kufanya usanifu wa kina wa barabara hii katika mwaka 2024/2025 kwa lengo la kutambua gharama halisi za mradi huu na ujenzi wake utategemea na upatikanaji wa fedha.