Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 2 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 29 2024-08-28

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga jengo la kisasa la Mahakama ya Wilaya ya Meatu?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania imeendelea kuimarisha majengo ya Mahakama katika ngazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kujenga majengo mapya na ya kisasa na kukarabati majengo chakavu. Wilaya ya Meatu ni moja ya wilaya ambazo zina majengo ya Mahakama lakini jengo lake ni chakavu na siyo la kisasa. Kwa mujibu wa mpango wa ujenzi wa majengo ya Mahakama, Wilaya ya Meatu itajengewa jengo la kisasa katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.