Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 2 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 32 2024-08-28

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga kiwanja cha michezo cha Kisasa Mkoani Njombe?

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Answer

NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali ipo kwenye ukarabati wa viwanja vya Uhuru na Benjamin Mkapa, ujenzi wa uwanja wa Arusha (Arusha Stadium) na kukarabati viwanja vingine vitano (5) vya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya CHAN 2024 na AFCON 2027. Kama sera ya michezo inavyoelekeza, ujenzi wa miundombinu ya michezo ikiwemo viwanja ni jukumu la Serikali ikishirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Mamlaka ya Serikali za Mitaa. Baada ya kukamilisha ujenzi wa viwanja kwa ajili ya mashindano ya CHAN 2024 na AFCON 2027, Serikali itatoa maelekezo kwa uongozi wa Mikoa yote ili kutekeleza mkakati wa ujenzi wa miundombinu ya michezo katika Mikoa yote. nakushukuru.