Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 54 Water and Irrigation Wizara ya Maji 701 2024-06-26

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: -

Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa miundombinu ya maji iliyochakaa na kusababisha upungufu wa maji – Chemba?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha huduma ya majisafi na salama wilayani Chemba, Serikali imekamilisha ukarabati wa Skimu mbili za Maji ya Songolo na Chemba Mjini katika mwaka wa fedha 2023/2024. Uboreshaji huo umerejesha huduma ya maji kwa wananchi 16,084 wa maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, vilevile, Serikali inaendelea na ukarabati wa Skimu za maji za Humekwa, Mlongia, Soya, Daki, Dalai, Gumbu, Kwamtoro, Kubi, Moto, Chinyika, Kelema Maziwani, Ovada na Churuku. Ukarabati wa skimu hizo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024 na kuboresha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi 13,770 wa vijiji hivyo.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imepanga kukarabati Skimu za maji za Kelema Balai na Khubunko utakaoboresha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi 7,906 waishio kwenye vijiji vitatu vya Kelema Balai, Kelema Mashariki na Khubunko katika Wilaya ya Chemba.