Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 54 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 702 | 2024-06-26 |
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: -
Je, lini mradi wa maji ya Ziwa Victoria kutoka Butiama kwenda Nyamuswa - Bunda utakamilika?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa mradi wa maji wa Ziwa Victoria ambao utatoa maji kwenye tanki la lita 2,000,000 la Mradi wa Mugango - Kiabakari lililoko Wilaya ya Butiama kwenda Bisarye mpaka Nyamuswa wilayani Bunda Mkoani Mara. Utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo kazi zinazotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa matanki mawili yenye jumla ya ujazo wa lita 500,000, ulazaji wa bomba umbali wa kilometa 23.1, ukarabati wa vituo 18 vya kuchotea maji pamoja na kuunganisha zaidi ya wateja 2,000 wa majumbani, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved