Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 54 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 703 | 2024-06-26 |
Name
Mrisho Mashaka Gambo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arusha Mjini
Primary Question
MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza:-
Je, lini mradi wa majitaka uliopo Kata ya Olmot ambao utaunganishwa na Kiwanda cha A to Z utakamilika?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA) inaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya uondoshaji majitaka wa Olmot utakaonufaisha Kiwanda cha A to Z pamoja na wakazi 1,200 wa maeneo hayo. Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 11.8, ujenzi wa nguzo 30 za kushikilia bomba kwenye vivuko na ujenzi wa Chemba 125 za ukaguzi wa mfumo wa majitaka.
Mheshimiwa Spika, hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved