Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 6 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 97 | 2024-11-05 |
Name
Neema Gerald Mwandabila
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NEEEMA G. MWANDABILA aliuliza: -
Je, kuna mkakati gani wa kupandisha kiwango cha mauzo ya kahawa kitakacholipwa benki badala ya shilingi milioni moja inayolipwa kwa sasa?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali iliweka utaratibu wa wakulima wanaouza kahawa kulipwa fedha za mauzo ya kahawa zaidi ya shilingi milioni moja kupitia akaunti zao za benki kwa madhumuni yafuatayo:-
(i) Kuondoa hatari za wakulima kuibiwa fedha zao za mauzo ya kahawa na kuhakikisha wakulima wanapokea fedha za mauzo kwa uharaka na usalama;
(ii) Kudhibiti upotevu wa fedha za wakulima kupitia vyama vya ushirika;
(iii) Kuongeza jitihada za kuwajumuisha wakulima wa kahawa kwenye mifumo rasmi ya fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali haina mpango wa kupandisha kiwango kinacholipwa kupitia benki kwa sababu kiwango hiki bado ni kikubwa na kinakidhi mahitaji ya lazima kwa wakulima. Kuongeza kiwango hiki ni kuongeza hatari za kiusalama na kufifisha azma ya Serikali ya kutumia mifumo ya kidjiti katika ulipaji wa fedha nchini.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved