Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 6 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 102 | 2024-11-05 |
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: -
Je, lini mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria wa Rorya - Tarime utakamilika kwa kuwa kasi ya utekelezaji ni ndogo sana?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka Rorya - Tarime unaendelea kutekelezwa na Mkandarasi CCECC kutoka nchini China pamoja na Mtaalamu Mshauri WAPCOS Limited kutoka nchini India. Kwa sasa utekelezaji wake umefikia 13%, kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita milioni tatu Mogabiri - Tarime Mjini; ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita milioni moja Sirari na ujenzi wa kituo cha kusukuma maji kinachojengwa eneo la Gamasara -Tarime Mjini. Mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Julai, 2025 na kunufaisha wananchi wapatao 729,496, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved