Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 5 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 83 | 2024-11-04 |
Name
Seif Khamis Said Gulamali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manonga
Primary Question
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: -
Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa miradi ya maji ya Ziwa Victoria katika Kata ya Igoweko, Uswayu na Tambalale – Manonga?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Seif Khamis Said Gulamali, Mbunge wa Jimbo la Manonga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kutambua umuhimu wa maji kwa ajili ya wananchi wake, inaendelea kutekeleza miradi mikubwa miwili ya kutoa maji Ziwa Victoria ambayo ni Mradi wa Ziba-Nkinga wenye kuhudumia vijiji tisa na Mradi wa Nkinga - Simbo utakaohudumia vijiji vinane. Mipango ya Serikali ni kusambaza maji kupeleka katika Kata ya Igoweko, Tambalale na Uswayu mara baada ya kukamilika kwa miradi hiyo. Aidha, Serikali inaendelea na zoezi la uchimbaji wa visima na kujenga miundombinu rahisi ya kuchotea maji (Point source) kwa ajili ya Igoweko, Mpogolo na Igondela vilivyoko katika Kata ya Igoweko, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved