Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 17 | Sitting 5 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 84 | 2024-11-04 |
Name
Josephine Johnson Genzabuke
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE: JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga soko la kuuzia Zao la Muhogo katika Mkoa wa Kigoma?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Johnson Genzabuke, Mbunge Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo katika Mkoa wa Kigoma imetenga eneo la ekari 4.26 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kuuzia zao la muhogo. Hivyo, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imepanga kujenga soko hilo katika mwaka wa fedha 2024/2025 baada ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kukamilika, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved