Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 55 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 710 | 2024-06-27 |
Name
Norah Waziri Mzeru
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NORAH W. MZERU aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia Wasichana wanaokatisha Masomo kwa sababu ya kupata ujauzito?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ahsante. Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha wanafunzi wasichana wanaokatisha masomo kwa sababu ya kupata ujauzito wanarejea shuleni. Hatua hizo ni pamoja na kutoa Waraka wa Elimu Na. 2 wa Mwaka 2021 kuhusu kuwarejesha wanafunzi waliokatiza masomo kwa sababu, mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito.
Mheshimiwa Spika, waraka huu umetoa fursa kwa mwanafunzi wa kike aliyepata ujauzito kurudi shule kukamilisha mzunguko wake wa kielimu ama katika shule yake ya awali au shule yoyote ambayo mzazi/mlezi na mwanafunzi watakubaliana na mamlaka husika kwa lengo la kuhakikisha mwanafunzi anakamilisha mzunguko wake wa kupata elimu. Vilevile, Serikali imeweka mfumo usio rasmi ambao unaruhusu mtu yeyote kujiendeleza kielimu, ili kukamilisha malengo yake, hususan katika Elimu ya Watu Wazima au vyuo vya maendeleo ya wananchi ambapo hata mwanafunzi aliyekatiza masomo anaruhusiwa kujiunga, ili kukamilisha mzunguko wake wa kupata elimu. Nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved