Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 41 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 533 2024-06-05

Name

Nicholaus George Ngassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. ANDREA K.n.y. MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa uzio katika Shule ya Sekondari ya Igunga?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2023/2024 Serikali imepeleka shilingi milioni 58 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na matundu matano ya vyoo katika Shule ya Sekondari Igunga kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Mwaka 2024/2025 Halmashauri ya Igunga kupitia mapato ya ndani imetenga shilingi milioni 55 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uzio katika Shule ya Sekondari Igunga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa uzio kwa ajili ya ulinzi wa mali na wanafunzi wa bweni, hata hivyo, kwa sasa kipaumbele cha Serikali Kuu ni ujenzi wa miundombinu ya msingi inayowezesha kuongeza nafasi za udahili wa wanafunzi.