Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 534 2024-06-05

Name

Hawa Subira Mwaifunga

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HAWA S. MWAIFUNGA aliuliza:-

Je, upi mkakakati wa Serikali kujenga mifereji kudhibiti mafuriko Tabora Mjini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya upembuzi yakinifu na usanifu wa mifereji mikubwa ya maji ya mvua katika Kata za Malolo, Mpera na Mwinyi ambazo zimekuwa zikikumbwa na mafuriko wakati wa kipindi cha mvua na kubaini kuwa shilingi bilioni 18.47 zinahitajika kujenga mitaro mikubwa yenye urefu wa kilometa 25 katika Mji wa Tabora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2022/2023 kiasi cha shilingi milioni 399.12 kutoka fedha za majimbo na tozo ya mafuta zilitumika kujenga sehemu ya mitaro hiyo yenye urefu wa kilometa 2.4. Pia katika mwaka 2023/2024 kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Miji ya Tanzania (TACTIC) itajengwa mifereji mipya kwenye Barabara ya Kisarika yenye urefu wa kilometa 2.99 ambapo barabara hii inaunganisha Kata ya Mwinyi na Malolo.