Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 41 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 538 2024-06-05

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani madhubuti wa kukomesha kabisa ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya watu wengi?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Felista Deogratius Njau, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeweka mikakati madhubuti itakayosaidia kukomesha ajali za barabarani ambayo ni kuifanyia marekebisho Sheria ya Usalama Barabarani ambapo muswada wa sheria umeshawasilishwa Bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza.

Pili, kuboresha miundombinu ya barabara na kuweka alama za matumizi ya barabara; tatu, kuandaa utaratibu wa kufunga mifumo ya TEHAMA barabarani ili kufuatilia na kudhibiti ajali; na nne, kuandaa utaratibu wa ukaguzi wa lazima wa vyombo vya moto ili kudhibiti ubora wa vyombo hivyo viwapo barabarani na kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kupitia vituo vya luninga na redio, elimu kwenye shule za msingi, sekondari na vyuo, vituo vya mabasi, vituo vya bodaboda na bajaji, vituo vya ukaguzi wa magari, shule za udereva na kutoa mafunzo kwa madereva wa Serikali, taasisi za umma na watu binafsi, nakushukuru. (Makofi)