Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 41 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 540 | 2024-06-05 |
Name
Josephat Sinkamba Kandege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalambo
Primary Question
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya katika Mji Mdogo wa Matai, Wilayani Kalambo?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Kalambo ni miongoni mwa wilaya zenye changamoto ya miundombinu chakavu ya Mahakama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa huduma za Mahakama ya Wilaya zinapatikana katika Jengo la Mahakama ya Mwanzo Matai. Aidha, zabuni ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Kalambo ambayo pia itajumuisha Mahakama ya Mwanzo ya Matai imeshatangazwa na ujenzi unatarajiwa kuanza mara baada ya kukamilika kwa taratibu za manunuzi, nashukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved