Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 51 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 651 | 2024-06-21 |
Name
Seif Khamis Said Gulamali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manonga
Primary Question
MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: -
Je, lini Serikali itazipandisha hadhi shule za Sekondari Manonga, Seif Gulamali, Simbo na Nkinga kuwa za kidato cha tano na sita?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Igunga ina jumla ya shule tano za kidato cha tano na sita. Tathmini iliyofanywa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI katika shule za Sekondari Manonga, Seif Gulamali, Simbo na Nkinga ilibaini kuwa shule hizo zina upungufu wa miundombinu inayohitajika kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita ikiwemo mabweni na bwalo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Igunga itatenga bajeti pamoja na kushirikiana na wananchi kukamilisha ujenzi wa miundombiniu inayohitajika ikiwa ni pamoja na kuomba kusajiliwa kwa shule hizo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia baada ya kukamilika ili ziweze kupandishwa hadhi na kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved