Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 51 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 653 2024-06-21

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: -

Je, hatua gani zinachukuliwa ili kupunguza changamoto ya walimu katika shule za msingi na sekondari mkoani Mara?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikifanya jitihada kila mwaka kuajiri walimu wa shule za msingi na sekondari. Katika kipindi cha mwaka 2020/2021 hadi 2022/2023, Serikali iliajiri walimu 29,879 wakiwemo walimu 16,598 wa shule za msingi na walimu 13,281 wa shule za sekondari. Mkoa wa Mara ulipangiwa walimu 754 wa shule za msingi na walimu 412 wa shule za sekondari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2023/2024 Serikali inatarajia kuajiri walimu 12,000 ambao watapangiwa vituo vya kazi katika maeneo yenye upungufu mkubwa ikiwemo Mkoa wa Mara.