Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 51 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 654 2024-06-21

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza:-
Je, kuna mpango gani wa kujenga mitaro ili kuzuia uharibifu wa barabara unaosababishwa na mvua katika maeneo ya milimani Mkoani Kilimanjaro?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kukabiliana na uharibifu wa barabara za milimani unaosababishwa na mvua, Serikali kupitia bajeti zake inahakikisha kuwa wakati wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara katika maeneo hayo, ujenzi wa mifereji unapewa kipaumbele ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege na ujenzi wa mikanda ya zege (concrete strips) katika maeneo yenye miinuko mikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2023/2024 shilingi bilioni 2.057 zilitumika kujenga mifereji yenye urefu wa mita 8,066, mikanda ya zege (concrete strips) mita 600 na barabara za zege mita 4,985 katika maeneo ya milimani katika Mkoa wa Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2024/2025 Serikali imepanga kutumia shilingi bilioni 2.077 kwa ajili ya kujenga barabara za zege mita 3,425, mikanda ya zege (concrete strips), mita 2,500 na mifereji ya maji ya mvua mita 2,250 katika maeneo ya milimani mkoani Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga bajeti katika miaka ijayo kwa ajili ya kujenga barabara za zege, mikanda ya zege (concrete strips) na mifereji ya maji ya mvua katika maeneo ya milimani Mkoani Kilimanjaro kulingana na upatikanaji wa fedha.