Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 51 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 660 | 2024-06-21 |
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:-
Je, kati ya mwaka 2021 – 2022 Serikali ilianzisha miradi mingapi mipya ya umwagiliaji ili kukuza kilimo cha mpunga katika Jimbo la Kilombero?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Kilombero ni miongoni mwa Majimbo ambayo yana maeneo makubwa yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji hii ikijumuisha bonde la Kilombero lenyewe pamoja na skimu ya Msolwa Ujamaa ambayo imefanyiwa ukarabati na kukamilika mwaka 2020/2021.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeingia Mkataba na Mshauri Elekezi Saba Engineering PLC kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika bonde la Kilombero ili kujua gharama halisi za kujenga miundombinu ya umwagiliaji kabla ya kuingizwa katika mpango wa ujenzi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved