Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 13 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 171 2024-04-24

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga kituo cha Polisi Kijiji cha Ashengai Kata ya Karansi – Siha?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Kata ya Karansi imeshatenga eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 2,023 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata ambacho kitajengwa kwenye Kijiji cha Ashengai. Ujenzi wa kituo hicho umeshaingizwa kwenye mpango wa ujenzi wa vituo vya Polisi vya Kata vitakavyojengwa kuanzia mwaka wa fedha 2024/2025 na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, ahsante.