Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 21 Water and Irrigation Wizara ya Maji 280 2024-05-08

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASISHA E. MAFUWE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza kutekeleza na kumaliza kero ya maji katika Jimbo la Hai aliyoitoa Mheshimiwa Rais wakati wa Kampeni?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Saasisha Elinikyo Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutekeleza maagizo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoyatoa mwaka 2020 wakati wa ziara Wilayani Hai ya kumaliza tatizo la maji katika wilaya hiyo, Serikali imekamilisha utekelezaji wa miradi sita ukiwemo Mradi wa Maji wa Kikafu - Bomang’ombe ambao umezinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango wakati wa ziara yake mwezi Machi, 2024, Mkoani Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukamilika kwa miradi hiyo kumeboresha huduma ya maji katika Mji wa Hai hususani kwa wakazi 63,049 waishio kwenye Kata tatu za Bomang’ombe, Muungano na Bondeni; pamoja na wananchi wapatao 41,963 wa Vijiji vya Kwasadala, Rundugai, Kawaya, Foo, Nshara, Uduru, Wari Ndoo na Wari Sinde, Isawerwa, Kimira, Mudio, Roo Sinde, Roo Ndoo, Mkombozi Kware, Uswaa, Mamba na Mungushi, Ngosero, Mbatakero na Chekimaji. Aidha, utekelezaji wa miradi mitatu ya upanuzi wa skimu za usambazaji maji inaendelea ili kumaliza tatizo la huduma ya maji katika Jimbo la Hai.